Ofa zinazotolewa mashuleni

kwa ujumla tunatoa vifaa na ujuzi wetu bure.Kama ulkipenda tunakutembelea katika vipindi vyako na kuonyesha picha pamoja na kujadili baadhi ya mada kuhusu Tanzania na wanafunzi wako.Pia kama inawezekana tunaweza kupanga ziara ya wageni kutoka Tanzania kuja kutembelea shule yako au kuingia kwenye vipindi.

Kama una swali lolote kuhusu Tanzania kwa ajili ya vipindi vyako kwa furaha tunatuma ombi lako kwa wa watu ambao wanafanya kazi za mazoezi nchini Tanzania .kwa njiia hii unaweza kupokea maelezo na picha zinazohusu maisha ya eneo la kilimanjaro nchini Tanzania.kwa ajili ya vipindi vyako.

Pia tunatoa mwongozo wa maonyesho yetu kuhusu Tanzania.Mahali popote tunapopata fursa tunatoa mwongozo huo na hata tukiwa pamoja na wageni wetu kutoka Tanzania.

Kama shule inataka kujua zaidi kuhusu mambo yanayofanyika katika uhusiano wetu na Tanzania wanakaribishwa katika vikao vya mtandao wetu.Ambapo tunaratibu mikutano yetu na safari zetu,Pia tunapokea mapendekezo ya mtu yeyote na kuunganisha mitandao tofauti kwa ajili ya kusaidiana na kufanya kazi pamoja.

Zaidi ya hayo watu wote wapya tunaoshirikiana nao kwa sasa katika mtandao wetu wanafursa ya kuingia katika ushirikiano wetu na Tanzania tuliokuwa nao toka mwaka 2003.Hii ina maana kwamba kuweka mawasiliano ambayo tunapanga na kufanya kazi pamoja na shule huko Kilimanjaro ambao tuliunda na kufanikiwa kupata na washirika wetu wa ndani.

Kama shule inataka kuingia kwenye ushirika na shule zaidi ya ushirikiano wa kawaida tulionao tunaweza kuwasaidia kwenye mawasiliano na shule hiyo ambayo wanataka kushirikiana nayo.

Kitu kingine ni kwa sasa RAFIKI wamenunua masanduku  tisa kwa ajili ya biashara ya haki (fair trade).Hii imeweza kuendelezwa na washirika wetu  BiBeKu GmbH.Ndani ya masanduku hayo kuna vitu vya aina mbalimbali ambavyo vinasaidia wanafunzi kujifunza mambo endelevu kwa  njia ambayo inavutia.Ndani ya masanduku hayo kuna vifaa vya kujifunzia,muvi na vitabu vyenye mada.

Nyuma