"Schule auf dem Weg"(shule njiani) - Kujifunza mambo ya kimataifa kama wito wa maendeleo ya shule

Kwanzia mwanzo wa mwaka 2013 shule ya RBZ Wirtschaft iliyopo Kiel. Inajaribu njia ambazo shule zinaweza kuchangia kwenye maendeleo ya kimataifa kwa mambo ambayo yatakuwa ni ya haki kwa jamii,mazuri kwa mazingira na ya uchumi mzuri wakishirikiana na shule nyingine mbili kutoka schleswig holstein, “Regionalschule am Himmelsbarg” kutoka eneo la Moorrege na shule ya “Gemeinschaftsschule am Lehmwohld” kutoka eneo la Itzehoe. Haya mambo ya maendeleo endelevu yanatakiwa kuhusishwa kwenye shule na kuwa kati ya vitu vinavyofanyika.

Kwa undani ni kuhusu kuhusisha maswali na changamoto ya maendeleo endelevu ya kimataifa kwenye masomo na katika maisha ya shule ya kila siku.

Kwenye shule zote makundi yalitengenezwa kutoka kwa walimu wa kawaida na wakuu ambayo yanahusika na utekelezaji wa mambo endelevu yanayotakiwa . na pia walimu na wanafunzi wengi iwezekanavyo wanatakiwa kuhusika. Mambo haya endelevu yanatakiwa kufanyika kwenye shule nzima ya “RBZ Wirschaft“iliyopo Kiel. Miradi ya kufundishia shuleni na vitendo inatakiwa kuchukua mada ya mambo endelevu.pia hadi kwenye mgahawa vyakula vinatakiwa kuhusisha mambo endelevu kama ya kimazingira na pia kuweka bidhaa ambazo zinazalishwa katika eneo hilo na kutumia teknologia ambayo haiharibu hali ya hewa.

Huu mradi umekuwa ukifanya kazi mpaka katikati ya mwaka 2015 na umekuwa ukisaidiwa na ENGANGEMENT GLOBAL GmbH ambayo inafadhiliwa na wizara shirikisho ya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo.

Nyuma

 

 

kwa ushirikiano na:

Imedhaminiwa na: