Kikundi cha kuimba cha RAFIKI 2012
Oliver Zantow
Sio kwa kukuza mambo tukisemakuwa ugeni wa mwaka huu ulikuwa wa mafanikio makubwa kama mambo ambayo tumefanya mpaka sasa. Tulikutana na watu wapya na pia kukutana na marafiki zetu wa zamani. Hii iliweza kufanyika kwa kuongea kwenye mtandao. Watu wengi waliweza kupata taarifa kuhusu hichi kikundi cha kuimba na kuweza kufika.
Kazi za kielimu/ushirikiano na shule
Oliver Zantow
Tulitembelea shule tisa tofauti kwenye eneo la Schleswig- Holstein. Shule hizo zilikuwa ni RBZ Wirtschaft Kiel, RBZ Steinburg iliyopo Itzehoe, Hannah-Arendt-School iliyopo Flensburg, Gemeinschaftschule Lehmwohld iliyopo Itzehoe, Gemeinschaftschule iliyopo Bad Segeberg ,Gemeinschaftschule iliyopo Kellinghusen, schule za Heikendorf na Großhansdorf kama schule ya msingi ya Kellinghusen. Tuliongea na wanafunzi na walimu kuhusu siku za zenye matukio na jinsi watakavyo jifunza na mambo mengine mengi.
Tulitembelea chuo cha Christian-Albrechts kilichopo Kiel, dhumuni la kufanya kikao ambacho kilihudhuriwa na wanafunzi,maprofesa na wanasayansi.
Tulitaka kufikisha taarifa kuhusu Tanzania kwenye shule za Ujerumani, kwahiyo tuliandaa taarifa na kuiwakilisha pamoja na vifaa ambavyo tulitoa kutoka Tanzania.
Kwenye kituo cha ufundi cha binafsi cha BiBeKu GmbH tulifanya kazi pamoja na wanafunzi wa chuo hicho cha ufundi.
Zaidi ya hapo, moja ya vitu ambavyo tulikuwanavyo kwenye ratiba yetu ni “uzoefu wa chakula”ikiwemo moja ya mambo endelevu, tulikuwa na tukio lenye mada ya kahawa.
Kwenye hili tukio wageni wetu ambao pia ni wakulima wa kahawa kwenye eneo la Kilimanjaro walihudhuria. Hili tukio lilipelekea kwa uamuzi wa kufanya Kellinghusen kuwa “mji wa biashara ya haki. Huu uamuzi uliafikiwa.
Uhusiano mwingine kwenye ngazi ya jamii ulikuwa kwenye eneo la Duisburg ambalo liko kama eneo la Hvide Sande lililoko Denmark.pia ilileta uwezekano mkubwa wa kufanya kazi pamoja.
Mwisho tunaweza kusema kwamba hii ziara ilikuwa ni nafasi nzuri kwa watu watakaokwenda Tanzani kwa kuwa waliweza kupata mawasiliano.
Wanachama wa kikundi cha RAFIKI
Imefadhiliwa na: