Vikao kwenye mtandao

Kwanzia mwaka 2012 tumealika watu ambao tunafanya nao kazi na pia shule zilizopenda kujumuika na sisi kwenye  vikao vyetu kwa mwaka.kwenye vikao hivi tunaratibu kazi zetu  na safari zetu tukihusisha watu wote tunaoshirikiana nao wakiwemo kutoka Tanzania.

Kikao cha mtandao mwaka 2015

 Rebecca Morsch

Kikao cha tano kilichofanyika kellinghusen tarehe 6 mwezi wa 7 mwaka 2015.

Kwanza kabla ya yote kulikuwa na utambulizi kuhusu maendeleo ya sasa ya shule ya KIUMAKO.Mwongeaji wa RAFIKI Bwana Oliver Zantow alisisitiza kwamba kulikuwa na mafanikio makubwa mwaka uliopita.Shule ya kiumako kuweza kupata usajili kutoka serikalini kuwa inatambulika kama shule ya sekondari.Pracseda na Gilbert Towo ambao ni moja ya wafanyakazi katika shule ya KIUMAKO walialikwa kama wageni rasmi.Gilbert Towo alitoa salamu na alifarijika kwa kuona namba kubwa ya vijana wadogo waliopo kwenye ushirikiano na RAFIKI.

Marcus Wack,ambaye ana wajibu wa kutunza vijana wa kujitolea kwa RAFIKIe.v alitoa taarifa kuhusu kazi ya vijana hao kwa sasa kwenye shule ya KIUMAKO na kwenye miradi ya ushirikaiano.Mbali na hayo vijana hao wanaofanya kazi ya kujitolea wawili kati ya wanne walitambulishwa.Caroline Parr na Charlotte Masekowsky.

Zaidi baadhi ya washirika wetu walituelezea kuhusu miradi yao.Anja kutoka kwenye shule ya Selma-Lagerlöf-Gemeinschaftsschule iliyopo Ahrensburg alielezea kuhusu mbio walizozifanya za kukusanya fedha na wanafunzi walikusanya euro 6.232 kwa ajili ya miradi ya rafiki Tanzania.Aliwasilisha hundi ya fedha hizo kwenye kikao hicho.

Kwa kuongeze Ellen na Klause Karpen walielezea kuhusu mpango mpya kuhusu jiko linalotunza nishati na ufahamu waliopata kutoka kwenye semina iliyotolewa na shirika la Artefact.Walileta jiko moja ili waweze kuonyesha watu na kuelezea.Baadae nyama ziliweza kuchomwa kwa kutumia jiko hilo.

Pia wafanyakazi wa BiBeKu GmbH Annika Ehlers, Isabella Seider and Nadja Lackmann walielezea kuhusu mradi ulioanzishwa wa kuuza vifaa vya kufundishia shule.Na pia walikuwa wameleta baadhi ya vifaa hivyo kwa ajili ya shule ndani ya mradi ambao walikuwa tayari wamenunua vifaa hivyo.

Baada ya hapo kulikuwa na muda wa kubadilishana mawazo kati ya washirika wa mtandao huo.

Mashirika yafuatayo yalikuwa kwenye kikao hicho:

Bibeku GmbH; AG Didaktik der Geografie, CAU Kiel; RBZ Steinburg; Jugend im Ausland e.V.; RBZ Wirtschaft . Kiel; GemS Lehmwohld, Itzehoe; GemS Himmelslbarg, Moorrege; BEI; Selma-Lagerlöf-Gemeinschaftsschule Ahrensburg; Ökopartner Kiel; Stadtmarketing Kellinghusen; KIUMAKO Secondary School.

Kikao cha mtandao mwaka 2014

Oliver Zantow

Kwanzia tarehe 23 juni mpaka 6 julai 2014 tulikuwa na wageni watano kutoka Tanzania.Mkuu wa shule ya ufundi KIUMO Fredi Minja,mchungaji Yese Kimaro,mfanyakazi wetu Pracseda Towo na pia wasichana wawili Gloria Mero na Nancy Towo.Wageni wetu hawakuudhuria tuu mkutano wetu uliohushs washirika wetu kama,Baadhi ya watu kutoka RAFIKI na pia wanafunzi kutoka chuo cha kiel kilichofanyika BiBeKu iliyopo Kellinghusen,Bali walitembelea pia baadhi ya shule katika ziara yao. GemSAm Himmelsbarg iliyopo Moorrege, GemS Am Lehmwohld iliyopo Itzehoe, RBZ Wirtschaft iliyopoKiel na RBZ iliyopo Steinburg.

Eneo la Moorrege, Itzehoe na Kiel waliweka siku za miradi kuhusu Tanzania ambazo zilikuwa na uhalisia mkubwa kwa sababu ya wageni waliokuwa wametoka Tanzania.

Kwa mfano mradi wa “activity day Tanzania“kwenye shule ya RBZ Wirtschaft huko Kiel ambao Fred na Yese walishiriki:

Fred Minja kutoka Tanzania alikuwa msemaji mkuu ambaye ni mkuu wa shule ya ufundi.Ni mtu ambaye alikuwa anajua vitu muhimu vya kuongea na ni mtu mzuri wa kufanya mazungumzo nae na ni mtu ambaye tulimtegemea.Na pia alikuwa anajua lugha ya kiingereza vizuri na ikawa ni mara ya kwanza ambapo wanafunzi wetu walipata shida kwa kuwa walitakiwa kuzungumza kiingereza.Baada ya muda kidogo na kutokuelewana mambo yalikuja kwenda vizuri.licha ya hayo pia mwalimu walikwepo muda wote ili kama watahitaji mtafsiri kwa wakati wowote.msemaji wa pili alikuwa Yese Kimaro.

Wanafunzi 15 wa darasa la awali la ufundi waligawanyishwa kwenye makundi matatu na walijifunza kuhusu maisha ya kila siku ya vijana wa Tanzania wakisaidiana na wageni kutoka Tanzania.walizungumzia ratiba za kila siku za hao vijana ,mambo wanayofanya kwa ajili ya kujifurahisha ,elimu na mafunzo ya ufundi kwa kulinganisha hizi nchi mbili.Zaidi walitafuta pia taarifa kutoka kwenye mtandao wakiongezea kwenye zile walizoambiwa na wageni kwa ajili ya maonyesho yao kuhusu Tanzania.

Majukumu yalikuwa kwa kiingereza na kijerumani.kwahiyo wageni kutoka Tanzania waliweza kushiriki vizuri na kuelewa mambo yaliyokuwa yanafanyika.Wanafunzi walikuwa na kazi ya kuandika kila kitu walichojifunza kwenye mabango kwa njia moja iliwasaidia wanafunzi kujifunza na pia mabango waliyotengeneza waliweza kuwaonyesha wanafunzi wengine wa hapo shule mambo waliyojifunza.Na pia watu wengine walipata taarifa hizi kutokana na mabango hayo.

Siku ya tatu wanafunzi walifungua mgahawa wao ambao unaitwa “Cafe Kilimanjaro“.Ambayo inauza bidhaa kutoka Tanzania na nyingine ambazo zimetengenezwa vizuri sio kwa kuweka madawa mengi.Hii ilikuwa fursa ya kwanza kuonyesha mabango hayo kwa wageni waliotembelea mgahawa huo.

Kuachana na hayo darasa lilichukua fursa ya kujadili mambo kuhusu ukuaji wa kahawa nchini Tanzania eneo la Kilimanjaro na maswali zaidi.

Kuongezea wageni wamejihusisha kwa ukamilifu kwenye uandaaji wa vijana wa kujitolea kwa RAFIKI kama sehemu ya mpango wa “Weltwärts“uandaaji huo ulifanyikia Kiel.

Pia wageni wetu waliweza kuhakikisha uandaaji wa hali ya juu kwa safari ya mwezi wa tisa au wa kumi kwa kutembelea shule.Ziara hiyo ya mashuleni iliyohudhuriwa na wawakilishi kutoka shule za Moorrege,Itzehoe na Kiel.pia wageni wetu walishiriki kwenge kikao cha kikundi tunachoshirikiana nacho cha huko RBZ iliyopo steinburg ambapo walianzisha mradi wa kuchimba kisima.

Maelezo haya machache yameonyesha kwa uwazi jinsi ambavyo ushirikiano na shule ya sekondari kiumako nchini Tanzania imehusishwa kwenye kazi za elimu kwenye eneo la Schleswig-holstein nchini Ujerumani.shule nyingine zimeonyesha kuvutiwa na ushirikiano huu kama shule ya Berufliche Schule iliyopo Bad Oldesloe.Shule ya  Gemeinschaftsschule iliyopo Ahrensburg na wakaamua kuweka uhusiano na shule ya kiumako kwenye mkutano wao wa shule.

Nyuma