Mradi wa asali
Kutumia rasilimali,kupata kipato:Asali ya Kilimanjaro
Na Oliver Zantow
Mradi wetu wa asali katika ushirikiano na mfugaji nyuki Eckhard Ranft kutoka kellinghusen.Ulifanikiwa kuanza vizuri na unatakiwa kuendelezwa.Marafiki zetu wa Tanzania walitoa hili wazo la kuwa na huu mradi wa asali na katika mradi huo rafiki zetu wa Tanzania walionyesha kuvutiwa sana.Hii inaweza ikaweka msingi tofauti kwenye uzalishaji wa asali.mradi huu wa asali unafadhiliwa na bingo.
Kwanza ningependa kusema maneno machache kuhusu mradi huu:Mfugaji nyuki Echard Ranft aliweza kufika Mrimbo/Tanzania na kukaa kuanzia tarehe 26 mwezi wa tisa mpaka tarehe 4 mwezi wa kumi mwaka 2014.Na aliweza kuzungumza na wafugaji kutoka Tanzania.
Mafunzo haya yalifanyika kwenye jengo la shule ya KIUMAKO ambalo tutapenda kulitumia kwa mafunzo ya ufugaji wa nyuki kwa wakati wote.Hii inahitaji sana uwekezaji na kupelekea uwezo mkubwa wa jengo na pia shule kukubalika kijijini.
Tulinunua vifaa ambavyo vinatumika UJerumani ambavyo havikuweza kupatikana Tanzania.Moja ya vifaa hivyo ni kifaa cha kutenganisha asali na pamoja na mzinga wa mbao ambao utatumika kama mfano ili tuweze kutengeneza mizinga mingine kama huo.Hii inamaana kwamba mafundi seremala wa mrimbo watakuwa sehemu ya maendeleo zaidi ya mradi huo.kwa mfano shule ya ufundi KIUMO.
Kwa bahati nzuri iliwezekana kutuma vifaa vilivyo nunuliwa kwenda Tanzania kwa makisio yaliyowekwa ya fedha bila kuzidi.Kiongozi wa maswala ya moto Hamburg ambaye anaushirikiano na shirika lililoko Dar alitusaidia kuandaa shehena hiyo.
Wafanyakazi tunaoshirikiana nao waliandaa mafunzo haya wakishirikiana na vijana wetu wa kujitolea kutoka mpango wa “weltwäts“.uwekezaji ulifanikishwa na mfugaji nyuki Thomas kutoka Tanzania ambaye awali hakujulikana kama mfugaji nyuki.
Kwanza kabisa Echard Ranft alipata wazo kuhusu hali iliyopo katika eneo la kilimanjaro.aligundua kwamba kuna nyuki wa aina mbili wanaweza kufugwa.Nyuki wadogo ambao hawaumi lakini wana mavuno kidogo.Hawa nyuki wanaweza kuwekwa kwenye mizinga ya nyumbani kwa kuwa hawana madhara.Kuvuna asali zega linatolewa na kukamuliwa.Hii inatengeneza juice tamu ambayo haifanani sana na asali.Ukiachana na hayo pia wingi wa nyuki unapungua.
Aligundua mbinu zinazotumika kwenye ufugaji wa nyuki ni moja kwenye nyuki wa kawaida na wakali pia.Baadhi ya wafugaji nyuki wanaweka mizinga kwenye mashamba yao na nyuki wanawekewa dawa kabla ya uvunaji na hii inaathiri nyuki hao.
Eckard alisindikiza kwenye kila kitu kilichokuwa kinaendelea .kwenye mazungumzo alitambua kuwa watu nchini Tanzania hawakujua kitu chochote kuhusu ufugaji wa nyuki.Hakukuwa na maarifa kuhusu malaika,wafanyakazi n.k.ila aliweza kujifunza kile alichokipata cha tofauti.
Mafanikio ya mwisho ni waliweza kupata kundi la nyuki ambao waliweza kuwaweka kwenye mzinga ambao uliletwa kutoka Ujerumani.kwa sasa mzinga huo wa nyuki upo KIUMAKO na kuvuna asali kunaweza kufanywa kwa kutoa fremu ya mzinga huo na kutoa asali.
Ukiachana na hilo kundi la nyuki lililopatikana linaweza kugawanywa ili tuweze kupata nyuki wengine zaidi.mbinu ya ufugaji wa nyuki ni rahisi kujifunza ,kitu kimoja ni kwamba Tanzania hamna vifaa vyote vinavyo hitajika.
Wafugaji wa nyuki katika eneo hilo kwa sasa wanajua mbinu muhimu za ufugaji nyuki na wamepewa ofa ya kutumia kile chombo cha kutenganisha asali bure.mradi huu umeweza kuanza kwa mafanikio.
Kwa sasa Eckhard Ranft anataka kukuza Zaidi mradi huu kwa kuanzisha shule ya kujifunza ufugaji wa nyuki katika shule ya KIUMAKO.Na yuko tayari kufanya kazi tena bila malipo yeyote.Kwa njia hii uzalishaji wa asali katika eneo la Kilimanjaro unaweza kufanyika kwa ufasaha Zaidi na kunaweza kukawa na mapato mazuri kwa wakulima.mahoteli yatafaidika kwa kuwa watalii watazidi kwa sababu ya hii.
Kukiwa na vifaa vinavyo hitajika,ufugaji wa nyuki wa asali unaweza kuleta mapato mazuri sana.
Imedhaminiwa na: