Mti kwa kila mwanafunzi

Upotezaji wa misitu ni tatizo la kimataifa na sana katika nchi masikini.karibia kila makazi kuna jiko linalotumia kuni. Na pia mbao zinatumika kwenye ujenzi. Jambo hili linatokea Tanzania pia.miti bado inakatwa bila mtu yeyote kufikiria kuhusu maisha ya baadae.

Kama hivi,miti ya aina ya mikoko inapotea kwa haraka sana maeneo ya pembezoni mwa bahari. Miti na misitu ambayo inaleta kivuli na ambayo inasaidia kuzuia mmomonyoko wa udongo inakatwa. Hata kwenye hifadhi za taifa miti inakatwa zaidi na zaidi.lakini watu katika makazi yao hawana budi kufanya haya kwa kuwa hawana njia nyingine. Hakuna ugawaji mzuri wa umeme na uhitaji unazidi kukua watu wanapoendelea kuongezeka. Juhudi kubwa itahitajika kwenye kuleta njia mbadala ambayo itasaidia kuweza kuondoa haya matokeo mabaya ya ukataji wa miti.sisi kama RAFIKI tunataka kushisiki kwa kile kidogo tunachoweza kufanya.RAFIKI imeanzisha ratiba ya kupanda miti kwa kila mwanafunzi ambaye anasoma kwenye shule ya KIUMAKO. Na kwa sababu ni wanafunzi wenyewe wanaenda kupanda tunachukua hii kama sababu ya kuwafundusha kuhusu utunzaji wa mazingira katika kila darasa.kwa kuwafundisha haya kuhusu mazingira pia wanaenda safari kwenye hifadhi za taifa na maeneo mbalimbali kujifunza na kuona kwa kuwa uharibifu wa mazingira unatokea dunia nzima:Na ni wale wanaojua asili ndo wanaoguswa kuitunza.

Nyuma