Majiko ya kutunza nishati kwa manispaa ya Moshi

Kuanzia mwaka 2013 kumekuwa na ushirikiano kati ya Kiel na manispaa ya Moshi. Mradi wa kwanza kwenye huu ushirikiano unakaribia kutambulika:kubadilisha na kuimarisha utumiaji wa amjiko ya kutunza nishati kwenye manispaa ya Moshi.RAFIKI e.v imekabidhiwa utekelezaji huo.

Watu wa eneo la kilimanjaro bado wanapika kitamaduni.wanapikia nje na kuni.Ifikapo kipindi cha mvua wanawasha jiko ndani au sehemu yenye bati.

Kutokana na moshi unaotoka kuna hatari kubwa ya afya.Na hatari hiyo inaongezeka zaidi pale ambapo wanapikia ndani. Zaidi ya hapo kunakuwa na uhitaji mkubwa wa kuni.kutokana na uongezekaji wa watu imekuwa shida kupata kuni.matokeo yake miti iliyoko shambani ambayo inaleta kivuli inakatwa na kazi inaongezeka kwenye uhifadhi wa mazingira.ukataji huo wa miti umesababisha uharibifu wa mazingira kwa kiasi kikubwa.maeneo mengi kwenye mteremko wa mlima Kilimanjaro kwa sasa yanapigwa na jua kwa sana.zaidi ya hayo kumekuwa na uharibifu wa udongo kutokana na ukuaji wa mahindi. Mmomonyoko wa udongo wakati wa mvua ni matokeo ya ukataji wa miti.mpaka sasa kuna eneo la kwenye mteremko limeanguka chini na kuna wajanga wa hili tatizo.kutoka na hayo mambo serikali imekataza kukata miti.lakini uhitaji wa miti bado uko pale pale. Miti iliyobaki imekatwa matawi yake na kubaki bila matawi.

Hili tatizo ni kubwa,kwa sasa mbao ni ghali sana na ni rahisi kutengeneza viti na chuma kuliko mbao.katika sehemu nyingi kuna mipango ya kupanda miti na RAFIKI ni mojawapo kati ya mashirika yenye mipango hiyo.Ina mradi wa “A tree for every student“.Lakini miti midogo inahitaji muda sana kukua ,mara nyingine inakauka au kuliwa na mbuzi.

Sambamba na majadiliano hayo ya kupanda miti mipya uhitaji wa kutumia njia nyingine ambazo ni nzuri kwa afya kwa kupika zinahitajika.

UTEKELEZAJI

Ni wajibu wetu kuwatambulusha watu wa Mrimbo kuhusu majiko.Majiko tofauti yanaonyeshwa na matumizi yake kwenye shule ya KIUMAKO na wanafunzi wanakua na ujuzi wa majiko hayo.

Katika miezi ya mwisho tulichukua nafasi kutembelea karakana tene na tena kutokana na teknolojia ya sasa.watu wawili kwenye shirika letu walishiriki kwenye karakana ya “Artefact“iliyopo Glücksburg na wakaweza kujua jiko zuri linaloweza kutunza nishati ambalo limejengwa na chuma ambazo hazishiki kutu.Limetengenezwa na wahandisi kwa matumizi ya Afrika kusini.

Haya majiko yana faida zifuatazo:yanahitaji kuni kidogo na pia yanapunguza uharibifu wa afya ya binadamu kwa kiasi kikubwa.Hii ni kwa sababu kuna mfumo wa kuingiza hewa kwenye jiko. Haya majiko ya kutunza nishati yataanza  kutumika kwa kiasi kikubwa.

Familia zilizoko eneo la Kilimanjaro zinaishi katika hali ya kawaida sana kwa sababu ni vigumu kuweza kufanikiwa kupitia mazao ya shambani .katika kusafirisha ndizi na kahawa na pia mboga mboga wanapata pesa ndogo ambayo ni ngumu kuweza kupata maendeleo(elimu,nguo au chakula)kwa familia zao.Hii inamaanisha majiko yanayo tunza nishati yenyewe hayawezi kubadilisha maisha ya kilasiku kwa sababu jiko lina gharama ya euro 50 ambayo ni zaidi ya mapato yote ya mwezi ya familia nyingi.

Kwa sababu ya hayo tutanunua majiko 100 na kuyagawa. Mji wa Kiel utashiriki gharama kwenye kununua . ugawaji utafanywa na usharika na utatekelezwa na KIUMAKO kama mradi wa kuelimisha .wanafunzi wataelewa teknolojia na maonyesho yatafanyika kuelezea watu kuhusu faida za majiko haya na kwa wakati huo huo kutimiza mahitaji ya KIUMAKO.mifano mbalimbali ikihusisha majiko yanayopunguza uhitaji wa kuni au ambayo yanaweza kutumia matakataka.KIUMAKO itatoa elimu sio kwa wanafunzi tuu bali kwa watu wazima watakaotaka pia kushiriki kwenye karakana.  Zaidi ya hayo manispaa nyingine zinaweza kuweka karakana bure.

Wanafunzi wa KIUMAKO wanaweza wakasambaza elimu kwa wanafunzi wengine wa eneo hilo na mkoa kwa ujumla.Umuhimu wa mradi huu ni kuchukua kizazi kichanga kuwaelezea hizi teknolojia na kuchukua hatua nzuri na kubadili mawazo yao kwa ajili ya baadaye.

Tumejadili mbinu kwa undani sana na kwa mifano na wawakilishi mbalimbali wa kanisa na serikali wakati tuliokuwa Tanzania.

Mradi ni kama ulivyoelezewa,ukisindikizwa na mradi wa “A tree for every student“kwa miaka tumepanda miti kwa kila mwanafunzi wa KIUMAKO.Huu mradi utakuzwa ili upandaji wa miti ufanyike na pia umuhimu wa misitu inaweza ikawa mada ya masomo katika shule ya KIUMAKO kwenye elimu endelevu.

Nyuma