Watu tunaoshirikiana nao

RBZ Wirtschaft . Kiel

Kwanza kabisa tuna ushirikiano mkubwa na RBZ Wirtschaft iliyopo mji wa kiel.Huko ushirikiano ni mkubwa sana hadi wameweza kufanikisha kujumuisha vipindi ambavyo wanazungumzia Tanzania kwenye ratiba yao ya vipindi vya kawaida.RAFIKI wanaandaa mashirika na uendelezaji wa miradi.Hii shule inatangaza project zetu na kazi tunazofanya kwa mfano kwenye,"cafe kilimanjaro". Mwaka 2009 mradi wa "Tanzania and me" ulianza huko schleswig-holstein.Ni kuhusu kukuza,kutambulisha na kushirikiana vitengo vya masomo.shule sita katika eneo hilo la schleswig-holstein zilihusika katika mradi huo.RAFIKI pia imeshirikiana katika huo mradi.

www.rbz-wirtschaft-kiel.de

Hannah-Arendt-Schule - Flensburg

Kwenye  shule ya Hannah-Arendt-Schule iliyopo Flensburg tumeanzisha ushirikiano ambao kwa baadae unaweza kusaidia kupata wanafunzi wa mazoezi ambao wataweza kwenda Tanzania.Pia tumetoa fedha ambazo zinaweza kusaidia mradi huo wa wakufunzi kuweza kufanya mazoezi Tanzania.

www.has-fl.de

AG Didaktik der Geografie am geografischen Institut der Christian-Albrechts-Universität Kiel

Ushirikiano mwingine tuliofanikisha ni kufanya kazi na kikundi cha Didact of Geography kilichopo kwenye chuo cha Christian-Albrechts-university Kiel.Dhumuni la ushirikiano huu  ni kukuza ukufunzi wa kimataifa katika ufundishaji wa walimu.Kufikia haya tunatoa walimu wa mazoezi kutoka chuo cha kiel kwa shule ya kiumako.Pia tunasaidia kuandaa vitu ambavyo waalimu hawa wa mazoezi wanaweza kuhitaji kama usafiri wao,malazi n.k.                                         

Kiukweli kazi yetu na shule ya kiumako inafaidika kutokana na uhusiano huu.

https://www.geographiedidaktik.uni-kiel.de/de

BiBeKu Gesellschaft für Bildung Beruf Kultur mbH - Kellinghusen

Tunashirikiana na BiBeKu GmbH.Hii taasisi ya binafsi inatusaidia kutunza wale vijana wa kutoka Ujerumani wanaojitolea kufanya kazi kutoka kwenye mpango wa"Weltwärt".Na pia kuwaandaa kwa kazi zao kabla ya kwenda Tanzania.Pia BiBeKu inaandaa mbio ambazo zinafanyika kellinghusen kwa ajili ya kukusanya fedha za mradi.Kwanzia mwezi wa pili mwaka 2015 BiBeKu inatunza ukurasa wa mtandaoni wa RAFIKI.

www.bibeku.de

Gemeinschaftsschule am Lehmwohld - Itzehoe

Kwa miaka mingi tumekuwa tukisaidia shule za schleswig-holstein na kuendeleza ushirikiano na Tanzania pamoja na utekelezaji wa masomo ya mada kuhusu Tanzania.Hii imepelekea mafanikio mazuri kwa mfano kwenye shule ya " Gemeinschaftsschule am Lehmwohld" iliyopo Itzehoe.Mara nyingi wageni kutoka Tanzania wamekuwa wakukaribishwa na kuweza kuwatembelea,kupata malazi n.k.Wanafunzi wa shule hii wameweza kuwa na miradi ambayo wameweka mada ya Tanzania na kuwa wanajifunza kuhusu Tanzania.Pia wameanzisha mradi wa"school on the way"kwa ushirikiano na RBZ Wirschaft,Kiel na Gemeinschaftsschule am Himmelsbarg,morrege.

 

gemeinschaftsschule-am-lehmwohld.lernnetz.de

Regionales Berufsbildungszentrum Steinburg - Itzehoe

Ushirikiano mwingine ni RBZ steinburg iliyopo Itzehoe walimu wa hii shule walitengeneza mfumo wa kupata umeme kutoka kwenye jua kwenye shule ya KIUMAKO(2012).Pia walitengeneza kisima cha kukusanya na kutunza maji kutoka kwenye mvua(2014) na wataweka mfumo wa umeme kutoka kwenye mimea na vinyesi vya wanyama(biogas)mwaka 2016.

 

www.rbz-steinburg.de

 Zukunft durch Sonne e.V. - Itzehoe

 

Tuna uhusiano na shirika la "Zukunft durch Sonne e.V." ambalo liliundwa kutoka kwenye kikundi cha wanafunzi cha RBZ steinburg.mwaka 2012 "Zukunft durch Sonne e.V."waliweka mfumo wa kupata umeme kutoka kwenye jua .mwaka 2014 walijenga kisima kwa ajili ya maji ya mvua.mwaka 2016 wanataka kujenga mfumo wa kupata umeme kutoka kwa mimea na vinyesi vya wanyama.

 

tansania.rbz-steinburg.de

Gemeinschaftsschule am Himmelsbarg - Moorrege

 

Kwa miaka mingi tumekuwa tukisaidia shule za schleswig-holstein na kuendeleza ushirikiano na Tanzania pamoja na utekelezaji wa masomo ya mada kuhusu Tanzania.Hii imepelekea mafanikio mazuri kwa mfano kwenye shule ya " Gemeinschaftsschule am Himmelsbarg " iliyopo moorrege.Mara nyingi wageni kutoka Tanzania wamekuwa wakukaribishwa na kuweza kuwatembelea,kupata malazi n.k.Wanafunzi wa shule hii wameweza kuwa na miradi ambayo wameweka mada ya Tanzania na kuwa wanajifunza kuhusu Tanzania. Pia wameanzisha mradi wa "school on the way"kwa ushirikiano na RBZ Wirschaft,Kiel  na Gemeinschaftsschule am Lehmwohld,Itzehoe

www.schulzentrum-moorrege.de

 Selma-Lagerlöf-Gemeinschaftsschule - Ahrensburg

 

Kwa miaka mingi tumekuwa tukisaidia shule za schleswig-holstein na kuendeleza ushirikiano na Tanzania pamoja na utekelezaji wa masomo ya mada kuhusu Tanzania.Hii imepelekea mafanikio mazuri kwa mfano kwenye shule ya "Selma-Lagerlöf-Gemeinschaftsschule" iliyopo Ahrensburg.Mara nyingi wageni kutoka Tanzania wamekuwa wakukaribishwa na kuweza kuwatembelea,kupata malazi n.k.Wanafunzi wa shule hii wameweza kuwa na miradi ambayo wameweka mada ya Tanzania na kuwa wanajifunza kuhusu Tanzania.Zaidi shule hii inasaidia kwenye kazi za RAFIKI kama kwenye mbio zilizofanyika kellinghusen 2015.

 

www.igs-ahrensburg.de