Kazi za kielimu

Miradi yetu inashughulika na kazi za kielimu kwenye shule nchini Tanzania na pia Ujerumani.

Kwa kutengeneza vifaa vya kufundisha,kuandaa maonyesho na kutoa ofa nyingine kama vifaa vya ufundishaji kwa biashara ya haki. Pia  tunaweza kusaidia shule mbalimbali kwenye mawasiliano katika mambo endelevu,biashara ya haki na mambo kuhusu Tanzania.

Nchini Tanzania kazi yetu muhimu ni kukuza kazi ya elimu kwenye shule ya sekondari KIUMAKO. Kwa mfano tunatangaza mradi wa “mti kwa kila mwanafunzi” na piakuwa na  michezo ya pamoja na wanafunzi kama ratiba ya mchana ni sehemu kubwa ya kazi yetu.

Kuachana na hayo miradi mingine mingi kwenye eneo la Kilimanjaro zinaweza kuonekana kwa kushirikiana na wengine kwa mfano tuliweza kuwafundisha wakazi wa eneo hilo la mrimbo jinsi ya kutunza nyuki na pia tuliweza kununua majiko ya kutunza nishati ambayo yanategemea kutumika siku za karibuni.