Weltwärts(kuelekea duniani)

Tangu septemba mwaka 2012 tumekuwa tunawapa nafasi wafanyakazi wa kujitolea kwa mpango wa serikali wa “weltwärts” kwa ushirikiano wa shirika linalowatuma hawa vijana wa kujitolea “JIA”(vijana nje ya nchi) Hawa vijana wa kujitolea wanafanya kazi kwenye shule ya KIUMAKO na kwenye miradi yetu.

Majukumu  

Kazi wanazofanya ni mbali mbali.unaweza kusaidia kama mwalimu wa kiingereza,kushiriki kwenye ukuzaji wa shule na kuandaa vitu vya kufanya baada ya shule kwenye kufanya kazi na vijana.

Msaidizi wa kufundisha

Moja ya kazi za vijana wa kujitolea ni kusaidia waalimu kwenye shule ya KIUMAKO wakati wanafundisha na pia kutoa masomo machache na klabu. Kwa mfano mwaka huu kuna klabu ya compyuta,kiingereza na kijerumani  na pia jiografia na hesabu. Kwenye shule ya watu wazima vijana hawa wanafundisha waalimu  mambo ya msingi kwenye kutumia compyuta na pia kiingereza.kutokana na hawa vijana wanavyopenda wanaweza kuendeleza klabu hizi au kuanzisha klabu nyingine kama wanavyopenda.

Kazi za mchana

Hata mchana kuna klabu tofauti zinazotolewa na vijana hawa wa kujitolea kwenye shule ya KIUMAKO. Hii inakuwa na michezo mbali mbali kama rugby,mpira wa miguu,mazoezi ya viungo na kucheza mziki. Hii ni kwenye klabu ya vijana ambapo wanafunzi wanapika pamoja,kucheza pamoja,kusaidiana kazi za shule,kuandaa safari,matukio ya jioni na mashindano ya michezo.zaidi ya hayo kulikuwa na bustani ya shule ambayo ilianzishwa na vujana wa kujitolea kwa kuotesha mboga pamoja na wanafunzi. Hapa pia vijana wa kujitolea wanaweza kuongeza kitu wanachopenda.

Kupika

Kwenye eneo la chakula bora kwa vijana wa Tanzania hawa vijana wa kujitolea wanasaidia kupika chakula cha mchana. Kwa kawaida inakuwa “ugali”(mahindi) na maharage. Vijana wa kujitolea wanaangalia mambo mchanganyiko kwa kupika na yenye virutubisho.

 

 

Nyuma

Mawasiliano:

Marcus Wack

marcus.wack(at)bibeku.de

 

 

kwa ushirikiano na: