Michango

Tunategemea sana michango ili tuweze kuendeleza shule yetu mpaka mwisho na pia kununua vifaa vya kufundishia.

Zaidi ya hayo tunataka kuwawezesha watoto wanaotoka katika familia masikini kuweza kwenda kwenye shule binafsi ambazo kwa kawaida ni ghali kwa kutoa ufadhili kwa baadhi ya wanafunzi. Katika mada hii ni  muhimu kujua kwamba serikali ya Tanzania inategemea shule binafsi lakini haisadii kitu chochote kwa hizo shule binafsi ama kwa pesa au kwa kutoa walimu. Shule ya sekondari KIUMAKO ni mali ya kanisa la Lutheran Tanzania lakini hakuna msaada wowote wa fedha kutoka eneo hilo.

Michango kwenye RAFIKI e.V. inakaribisha !

Akaunti ya benki

IBAN: DE57222500200040023003  

BIC: NOLADE21WHO

Sparkasse Westholstein

Na pia unaweza kupewa risiti ya uchangiaji.Tunaomba uwasiliane na mhazini wetu Werner Kaufmann kwa ajili ya hilo. (familiekaufmann(at)t-online.de).

uchangiaji wa fedha

Njia nyingine ya kusaidia ni kukusanya fedha kwa kuandaa vitu ambavyo vinaweza kutusaidia kukusanya fedha kama kukusanya chupa za plastiki ambazo ukirudisha dukani unapata fedha,mbio za kukusanya fedha au kuchangia vifaa.

Ukusanyaji wa hizo chupa na uandaaji wa boksi au chombo ambacho kina maneno ambayo yanaonyesha ufadhili wa chakula cha mchana kwenye shule  kwa pesa inayopatikana na kurudisha chupa hizo.

Jambo jingine ni kama kukimbia na kukusanya fedha ambayo inaweza kuandaliwa na shule mbalimbali na pia klabu za michezo.na kwa hizi mbio sehemu kubwa zinahitajika.

Zaidi ya uchangiaji wa fedha pia uchangiaji wa vifaa kwa watu wa Tanzania.watu wanakusanya vitu na vinapelekwa.uchangiaji huu wa kujitolea vifaa watu wanatoa kwanzia vitu vya majumbani ,vifaa vya michezo na pia vifaa vya hospitali.kama mtu anachangia kifa chochote vinakusanywa kwenye eneo la “lager und logistics”(stoo na vifaa) linalomilikiwa na BiBeku-JAW Steinburg liliyopo mtaa wa Oelixdorferstr.2.in 25524 Itzehoe.

Nyuma