Historia

Februari 2002 siku za miradi zilianza kwenye shule ya Ludwig-Erhard. Mojawapo ya miradi iliyotolewa ilikuwa ni kuhusu biashara ya haki chini ya kichwa cha habari “dunia moja “. Duka la dunia moja kwa biashara ya haki lilitembelewa ,kulikuwa na taarifa kuhusu usafirishaji bidhaa na kulikuwa na majadiliano na waziri aliyekuwa anahusikana eneo hilo Klaus Müller. Mwisho Helmut Krieg kutoka Heikendorf aliongea kuhusu miradi ya msaada kwenye eneo la Kilimanjaro ambayo ilikuwa imeanzishwa na usharika wa heikendorf kwa miaka mingi.

Kutokana na hayo wazo la kuwa na ushirikiano na shule ya eneo la mrimbo ulianzishwa.

Wakati wa siku ya “SCHILF”(Schulinterne Lehrerfortbildung = school intern teacher training)mwezi wa sita 2002 kikundi cha wanafunzi wa shule ya Ludwig-Erhard walishughulika na ushirikiano ambao ulikuwa umeanza na mawazo na mapendekezo kwa mada kwenye kufundisha Mwaka 2002 Loveland Makundi (kwa wakati huo alikuwa meneja wa shule ya ufundi ya KIUMO )na mchungaji panga (msemaji wa bodi ya KIUMO)walitembelea shule .walikuwa wageni wawakilishi kwenye eneo la Heikendorf. Na walikubaliana kukuza uhusiano ndipo wageni hawa wakamkaribisha Oliver na watu wengine kuja Tanzania ili kuona hali halisi.from this time on Oliver Zantow aliweka mawasiliano ya karibu kwa njia ya habari pepe kwa Loveland Makundi.

Septemba 2003 ziara ya kwanza kwenda Mrimbo ilifanyika. Ulrike na Rainer Kroggel pia Andrea Belitz na Oliver Zantow walisafiri kwenda Tanzania na wajumbe wa bodi ya KIUMO,ushirikiano huo ulianza rasmi.

Mwaka 2004 warsha ya waalimu ilifanyika Mrimbo .Nicole Hegedüs, Kathrin Pielsticker, Oliver Zantow (wote walikuwa wafanyakazi kwenye shule ya Ludwig-Erhard)na pia  Andrea Belitz alishiriki. Andreas Schweitzer alishughulikia compyuta za KIUMO na kwa wakati huo huo alijenga mtandao na kuweka kozi za elimu kwa ajili ya  walimu na wanafunzi wa ukarani katika shule ya ufundi ya KIUMO.

Mwisho wa hii safari ya Tanzania marafiki wetu waliomba msaada wa kujenga shule mpya ya sekondari.Elimsu Towo,Gilbert Towo na Oliver zantow walitafuta eneo ambalo linaweza kutumika kwa kujenga shule hiyo. Eneo hilo lilifanikiwa kununuliwa na ukurasa mpya kwenye ushirikiano wetu ulifunguliwa.

Mwezi wa sita mwaka 2005 wageni wa kwanza kutoka Tanzania walikuja ujerumani. Hawa wageni waafrika walikaa kwenye kituo cha vijana Kellinghusen. Na kufanya ziara tofauti tofauti na wenyeji wao kwa mfano kwenda Hamburg,Berlin,kisiwa kidogo cha ujerumani (Nordstrandischenmoor) na pia mgodi wa kutoa udondo wa simenti kama maeneo mengine ya vivutio yaliyopo eneo la Kellinghusen.

Mwezi wa kumi mwaka 2005 safari nyingine ilifanyika. kwa huu muda wanafunzi wa shule ya Ludwig-Erhard walienda Tanzania.vitu vilivyofanyika ni kuweka jiwe la msingi. Katika shule ya msingi KIUMAKO. Kuanzia hapo jengo lilianza kusaidiwa na Ujerumani.popote ilivyo wezekana. Mwanzo kabisa kutoka kwenye maeneo ya Kiel na Kellinghusen.

Mwaka 2006 shirika la RAFIKI lilianzishwa na kuanzia hapo ilikuwa inashughulika na mambo yote kwenye ushirikiano huo. Hii ina maana kwamba RAFIKI e.v. imekuwa ni shirika lililosajiliwalisilo la kujipatia faida kutokea mwaka 2006.

Mei 2009 warsha iliyopewa jina la “imba Afrika”ilifanyika na marafiki 7 kutoka Tanzania walishiriki kuelezea kuhusu maisha na tamaduni zilizoko kwenye eneo la Kilimanjaro. Zaidi ya hayo wanafunzi wa shule ya KIEL walifanya maonyesho kuhusu Tanzania pamoja na wajumbe wa shitika la RAFIKI.

Juni 2009 mbio za kwanza za uchangiaji wa fedha zilifanyika Kellinghusen na washirika kwenye  mtandao wetu BiBeKu(kituo cha vijana steinburg) zaidi ya washiriki 1000 kutoka shule mbali mbali za Itzehoe,Kellinghusen na kiel walijitokeza kushiriki ili kusaidia ujenzi wa shule ya KIUMAKO. Tangu hapo mbio hizi zinaandaliwa mara moja kwa mwaka.

Ili kuandaa ziara nyingine ya chuo cha Kiel Oliver Zantow,Martin Seemann na Marcus Wack(kutoka RAFIKI)na pia prof.Hoppe na mwalimu mwingine Ben Furkman walisafiri kwenda Tanzania mwezi wa 10 mwaka 2010.

Mwaka 2010 RAFIKI ilipokea tuzo ya miaka kumi ya elimu kwa maendeleo endelevu na UNESCO.

Mwezi wa sita mwaka huo mbio za kukusanya fedha zilifanyika Kellinghusen kwenye eneo la soko.

Mwaka 2011 chuo cha Kiel kiliandaa ziara ya kwenda Tanzania na wanafunzi na profesa wa taasisi    ya geografia kwenye chuo cha Christian-Albrechts chini ya mwongozo wa Oliver Zantow. Kuachana na Mrimbo kikundi hichi cha watu 42 walitembelea mkoa wa Dar-es-salaam,mkoa wa Arusha,Moshi,ngorongoro kreta na kisiwa cha Zanzibar.

Mwaka 2011 RAFIKI na BiBeKu waliandaa mbio za tatu za kuchangia fedha  Kellinghusen kwa mradi wa ujenzi wa shule.

Mwaka 2012 RAFIKI kwa mara ya pili ten ilipokea tuzo ya miaka kumi ya elimu kwa maendeleo endelevu kutoka UNESCO.

Baada ya miezi 18 ya kujiandaa wanafunzi wa RBZ Steinburg waliweza kuweka mfumo wa umeme wa jua kwenye jengo la KIUMAKO.mnamo mwezi januari 2012.

Mbio za kuchangia fedha za mara ya nne zilifanyika tena Kellinghusen na zilikuwa na washiriki 1000.

RAFIKI imekuwa mshirika rasmi kwenye shirika ambalo linapeleka vijana nje ya nchi kwa kufanya kazi za kujitolea(“JUGEND IM AUSLAND”)kwa mpango shirikishi wa “Weltwärts” kuanzia mwaka 2012 vijana wa kujitolea walianza kufanya kazi kwenye shule ya KIUMAKO.

Mwezi wa sita mwaka 2013 mbio za tano za kuchangia fedha zilifanyika Kellinghusen.Wanafunzi wa shule mbalimbali za Kellinghusen walishiiriki tena.walikuwa takriban wanafunzi 1000.

Kama timu ya kwanza kutoka Ulaya ya mpira wa miguu ya wanawake VFL kutoka Kellinghusen walisafiri kwenda Tanzania mwezi wa saba mwaka 2013.Walisafiri na kutembelea maeneo yaliyopo Afrika mashariki. Na kucheza mpira dhidi ya timu nyingine za wanawake. Dar-es-salaam,Zanzibar,Arusha na Moshi. Pia walicheza dhidi ya timu ya wanafunzi ya KIUMAKO na chuo cha ufundi KIUMO.

Vijana wane wa kujitolea walienda Tanzania mwezi wa tisa 2013 kwa kupitia mpango shirikishi wa Weltwärts kufanya kazi kwenye shule ya KIUMAKO Mrimbo kwa mwaka mmoja.

Mwezi wa pili wanafunzi na waalimu kutoka kwa washirika wa mtandao wetu RBZ Steinburg walienda Mrimbo kwa mara ya pili.Kwa ajili ya kujenga kisima kipya cha maji na pia kwa kuongezea hapo vifaa vya kusafisha maji kwenye eneo la KIUMAKO.

Mwezi wa sita mwaka 2014 mbio za sita za kukusanya fedha zilifanyika Kellinghusen eneo la soko.Idadi ya wanafunzi takribani 1000 walishiriki kwa mfano;kutoka shule zote za Kellinghusen,kwa ajili ya ujenzi wa shule ya KIUMAKO.

Kama timu ya kwanza ya mpira wa miguu ya wanawake ulaya Vfl kutoka Kellinghusen walisafiri kwenda Tanzania mwezi wa saba 2013. Walisafiri na kutembelea maeneo yaliyopo Afrika mashariki na kucheza mpira Dar-es-salaam,Zanzibar,Arusha na Moshi dhidi ya wachezajoi wa mpira wa miguu wa ndani. Pia walicheza dhidi ya timu ya mpira ya KIUMAKO na chuo cha ufundi KIUMO.

Vijana wane wa kujitolea walienda Tanzania mwezi wa tisa mwaka 2013 kwenye mpango shirikishi wa weltwärts kufanya kazi kwenye shule ya KIUMAKO Mrimbo kwa mwaka mmoja.

Mwezi wa pili wanafunzi na waalimu kutoka kwa washirika wetu wa mtandao wetu RBZ Steinburg walienda mrimbo kwa mara ya pili.walijenga kisima kipya cha maji.na kwa kuongezea waliweka vifaa vya kusafisha maji katika eneo la KIUMAKO.

Mwezi wa sita mwaka 2014 mbio za 6 za kukusanya fedha zilifanyika kellinghusen eneo la soko. Idadi ya wanafunzi takribani 1000 walikimbia kwa mfano:wanafunzi kutoka shule zote za Kellinghusen.kwa ajili ya ujenzi wa shule ya KIUMAKO.

Mwezi wa tisa mwaka 2014 vijana wengine wa kujitolea walienda KIUMAKO kwa msaada wa mpango shirikisho wa weltwärts.vijana wane walikaa mwaka mmoja kwenye shule ya KIUMAKO na kupata ujuzi kwenye miradi ya kushirikiana.

Pia mwezi wa tisa mwak 2014,mfugaji nyuki Eckard Rnft aliandaa warsha kuhusu nyuki,asali na ufugaji wa nyuki kwenye shule ya KIUMAKO. Wakazi mbalimbali wa eneo hilo walishiriki.

Mwisho wa mwaka 2014 shule ya kiumako ilipokea utambulisho kutoka serikali ya Tanzania kuwa shule ya sekondari na imekuwa ikiitwa KIUMAKO kwanzia hapo na mpaka sasa.

Mwezi wa tisa 2014 vijana wengine wa kujitolea wanne walipelekwa mrimbo kukaa mwaka  mmoja kwenye shule ya KIUMAKO kwa mpango shirikishi wa weltwärts.

Nyuma