Mpira wa miguu,darubini,biashara ya haki:safari ya Tanzania

kutoka kwa Marcus Wack (Agasti 2013)

Hii haijawahi kutokea kabla:timu nzima ya wanawake ya mpira ilisafiri kwenda Tanzania na kucheza mpira na timu za wanawake wa Tanzania.kwa kufanya hivi walikusudia kuimarisha wanawake wa Tanzania. Timu hii ya mpira ya wanawake vfl kellinghusen ilisafiri kwenda Dar es salaam,kwenye kisiwa cha Zanzibar,Arusha,kwenye  hifadhi mbalimbali za wanyama kama ngorongoro na Kilimanjaro. Lengo lilikuwa kwenye ujengaji wa shule ya sekondari ambayo ilijengwa na RAFIKI ikishirikiana na watu wa Tanzania na inafadhiliwa na watu wa Kellinghusen.wachezaji hawa wa mpira walipokelewa na ubalozi wa Ujerumani Tanzania pamoja na benki ya kwanza ya wanawake.

Mradi huu ulifadhiliwa na inter alia,Bingo-Lotto,huduma ya maendeleo ya wakristo na pia eneo la Schleswig-Holstein. Kuachana na hayo kampuni kama Autohaus Hellwig+Fölster GmbH, BiBeKu GmbH na pia Hummel Sport & Leisure GmbH waliwaunga mkono. Kwa kuongezea kwa asilimia kubwa timu iligharamikia safari hiyo kwa kuandaa matukio mengi miaka iliyopita. Oliver Zantow na Marcus Wack wa shirika la RAFIKI e.V. walipanga hiyo safari kwa kuwa walishaenda na wanafunzi wengi Tanzania kabla .kwenye upande wa Tanzania aliandaa Gilbert Towo ambaye ni guide aliesomea na ni mshirika wa RAFIKI pia.

 

Kuwasili: Wrist – Daressalam

Kwenye kituo cha treni cha Wrist safari ilianza kuelekea Hamburg ,Frankfurt,Addis Abeba mpaka Dar es salaam ambayo ilichukua masaa ishirini. Wazazi,marafiki na pia waandishi wa habari kutoka NorddeutscheRundschau walikuja pamoja kwenye uwanja wa ndege kusema kweheri kwa hawa wachezaji 23 waliokuwa wanasafiri kuroka kellinghusen kwenda Afrika mashariki. Zaidi ya hayo vyombo vya habari vya NDR na RSH walitoa taarifa kuhusu safari yetu. Kila mchezaji alikuwa na begi la pili ambalo lilikuwa na uzito wa kilo 25 kwa ajili ya kuweka vifaa vya shule ya KIUMAKO,madarasa ya awali,shule ya ufundi na pia kwa ajili ya klabu za michezo.

Sehemu ya 1: Daressalam

Kituo cha kwanza cha safari yetu kilikuwa Dar es salaam,mji mkuu wa Tanzania wa zamani na mji ambao bado ni mkubwa Tanzania.

Tulikaa kwenye hoteli nzuri ambayo ipo Kigamboni karibu na ufukwe wa bahari.tulianza kuangalia mechi zetu mbalimbali na kuanza kutembelea maeneo mbalimbali

Kwenye michezo tulikuwa na mechi inayovutia dhidi ya timu ya sayari queens F.C. kutoka Dar es salaam ambayo inaongoza. Hii timu yenye mafanikio makubwa ya wanawake wenye nguvu ambao baadhi yao walishakuwa ulaya na kucheza kwenye ligi za Uturuki na Swiden. Kwenye hali ya hewa ambayo sio ya kawaida ya vfl wakiwa wamechoka hawakuweza kufanya kufanya mengi kwenye hii mechi dhidi ya hii timu ya Afrika. Jule Mohr aliweza kupunguza magoli kwa kufunga goli dakika ya 56 lakini mwisho hii timu ya Afrika ilifunga 9:1. Uandaaji wa mechi hii ulikuwa wa kuvutia.mechi hii ilifanyika kwenye uwanja wenye majani bandia wa timu ya taifa (TFF). Refa wanne waliongoza mpira na waandishi wa magazeti mbalimbali walikuwepo na pia EA-TV.kuanzia mchana huu hawa wachezaji hawakuwa na shaka kwamba wako vizuri.kulikuwa na kapteni wa timu ya Tanzania “Twiga Stars”.

Zaidi ya kucheza mpira wa miguu na kuongea kwenye ubalozi wa Ujerumani,benki ya Tanzania ya wanawake(TWB),pia kutembelea soko la samaki jijini ilikuwa moja ya ratiba.kwahivyo wavuvi na wauza samaki walituongoza kwenye soko la samaki Dar es salaam na kuelezea kazi zao tofauti. Ilikuwa nzuri sana.mkuu wa benki ya wanawake TWB pamoja na msaidizi wake walituelezea kuhusu wazo la miradi wao.ukiachana na hayo pia tulipokelewa kwenye ubalozi wa ujerumani mmoja wa wafanyakazi alituelezea mambo mengi. Tuliweza kuangalia maisha ya jijini kwa kuwa tulitembea. Kwakuwa ilikuwa kipindi cha ramadhani ilikuwa ngumu kupata sehemu ya kula kwenye jiji la Dar.

Sehemu ya 2: Sansibar

Kisiwa cha viungo Zanzibar ilikuwa sehemu yetu ya pili.kwenye hichi kisiwa ambacho kimejaa waislamu tulikuwa na mechi yetu ya pili.ilikuwa vizuri sana na ya kushangaza kwa kuwa moja ya timu tano ilikubali kucheza katikati ya ramadhani. Walitaka kucheza dhidi yetu.ziara yetu ilikuwa nzuri sana kwa kuwa waziri wa michezo alikuja uwanjani kabla filimbi haijapigwa akashika wachezaji wote mkono na kuwakaribisha.

Kwenye timu ya New Zanzibar queens nane kutoka Zanzibar na wawili kutoka timu ya taifa Tanzania bara.mwisho ilikuwa 1:1.goli la VFL lilifungwa na Tine Peters. Baada ya mechi tuliwapa sanduku lenye vifaa vya michezo kama jezi,viatu,mipira n.k.zaidi kwenye hii hali tulijisikia tupo kwenye moja ya eneo masikini duniani.

Tulifurahi sana kuona shamba la viungo,kuongea na wakulima,kwenda kwenye kisiwa cha wafungwa,kutembelea jumba la sultani wa zamani na kuona mji wa kiarabu wa stone town wenye kanisa kuu la daiyosisi,soko la watumwa na pia jumba la makumbusho. Hii ilitupa mtazamo kwenye mabadiliko ya historia kwenye hiki kisiwa.

 
 
 
 

Sehemu ya 3: Arusha

Tulikwenda na ndege kutokea Zanzibar kuja Kilimanjaro kwenda kwenye mji wa Arusha. Mda ulikuwa mdogo na tulikuwa tumepanga safari kwenda kwenye mbuga za wanyama.

Mechi ilifanyika masaa 48 baada ya Zanzibar nje kidogo ya mji wa Arusha dhidi ya Testemony Sports Academy kwenye uwanja wa mchanga na hii timu ilifunga 2.0. mashabiki walikuwa wengi na baada ya mechi walikaa pamoja nakula na kusherehekea kwa pamoja na watu tofauti tofauti

Kwenye kuandaa safari wachezaji walifanya ziara ya kutembea na safari ndogo kwenye mbuga ya wanyama ya Arusha.kwa mara ya kwanza tuliweza kupata hali ya hewa ya ya baridi kwenye muinuko na kuona wanyama wa kwanza kama twiga ,pundamilia na nyati.

 
 

Sehemu ya 4: Mto wa Mbu na Ngorongoro

Safari iliendelea mpaka mto wa mbu na hifadhi ya ziwa manyara kwa kutumia usafiri wa gari na sehemu nyingine wa baiskeli.wasichana wa timu ya mpira ya VFL waliona tembo,nyati,viboko,pundamilia na pia chui na kwa mda mwingine wanyama walikuwa karibu sana.

Hakukuwa na mechi zozote zilizopangwa kwenye eneo hili. Hata hivyo ilitokea mechi ya ghafla kwenye mji wa Mto wa mbu kwenye eneo ambalo halina majani.wakati wa matembezi  walikuta wavulana wanacheza mpira na hawakutaka iwapite.walicheza na ilikuwa nzuri sana.kwenye tafrija zote tulizokuwa nazo hii ilikuwa ya kuvutia.

Tulitembelea wamakonde wanaochonga vinyago,wamaasai ambao wanaishi na mila zao na tulikula chakula cha jioni kwenye familia ya kitanzania ambayo ina watu wengi na ilitufundisha kujua jishi familia za kitanzani zinavoishi katika eneo hili.

Moja ya safari yetu ilikuwa pia kwenda Ngorongoro kreta. Baada ya kukaa Mto wa mbu tulitembelea hifadhi ya Ngorongoro kwa siku mbili.kwanza tulikaa kwa usiku mmoja kwenye iliyopo mwinuko wa mita 2300 juu ya kwenye mzunguko wa kreta. Jioni tulitembelewa na tembo na nyati kwenye mahema yetu. Tulikuwa na ulinzi wa wamasai na kula chakula kizuri cha eneo hilo na pia hali ya hewa ya usiku ilikuwa baridi kama digrii 0 na pia usiku ulikuwa mfupi sana.ila tulifurahi sana kwa kuona wanyama wakiwa kwenye kreta. Wengi wetu ilikuwa ni mara ya kwanza kuona vifaru na simba mbugani

 

 
 
 
 

Sehemu ya 5: Kilimanjaro

Mwisho wa safari yetu kwa baadhi ya tuliokuwa nao ilikuwa kama kwenda nyumbani.safari ya siku moja kwa kutumia gari kufika Mrimbo ambayo ipo kwenye safu ya mlima Kilimanjaro. Kwenye hili eneo Oliver na Marcus na pia kiongozi wa safari yetu Gilbert Towo wanasaidia ujenzi wa shule ya sekondari KIUMAKO na pia kazi kwenye miradi tofauti tofauti ya kwenye eneo la Kilimanjaro kwa miaka mingi kupitia shirika la RAFIKI e.V..Gilbert amezaliwa na kukuwa kwenye hili eneo na kwa sasa yupo kwenye miradi mingi ambayo ni ya kijamii. Baada ya kwenda sana pamoja na ujenzi wa shule Oliver na Marcus wanajisikia wapo nyumbani wakiwa mrimbo.

Tulifanya ziara kwenye kijiji hiki,kutembelea mashamba na pia shule za msingi, sekondari na chekechea na pia tuliweza kujiunga kwenye kupanda miti pamoja na wanafunzi na hii ilitusaidia kuona maisha mengine ya kulasiku ya watanzania.

Tulicheza mpira mara mbili.Moshi tulicheza na kufunga 5:0 dhidi ya timu iliyokuwa imepangwa na mechi nyingine ilikuwa dhidi ya wanafunzi wa kike kwenye shule ya sekondari KIUMAKO kukiwa na washabiki wengi.hii ilikuwa mechi ya kirafiki.baada ya kucheza Moshi tulitembelea kiwanda kikubwa cha sukari.pamoja na timu pinzani.

Tulichukua siku moja nzima kugawanya vifaa vya msaada mashuleni,hospitalini,chekechea n.k.kwenye makundi madogo ya wachezaji watatu tulitembelea mashirika tofauti tofauti na pia miradi tofauti pamoja na rafiki zetu wa Tanzania

Mwisho wa safari yetu sherehe kubwa iliandaliwa na wenyeji wetu kijijini Mrimbo.Marafiki zetu wa Tanzania na washirika wetu pia walikuwepo  na ikawa kama sherehe za wachaga.kulikuwa na ndafu na Dj ambae aliweka nyimbo za kitanzania.tulisherekea na kucheza mpaka asubuhi

 

 

Nyuma

 

 

Imefadhiliwa na: