Dhana za ufundishaji

Kwenye sheria inayotuongoza inasema:

“Kutokana na mahitaji ya agenda ya 21. Binadamu wanatakiwa kuwezeshwa kuweza kupambana na changamoto za utandawazi na kutengeneza dunia kwa kutumia elimu kuhakikisha maendeleo endelevu.

RAFIKI e.v. inahisi kuwa ina wajibu kwenye agenda ya 21 na ni lengo letu kujumuisha mambo ya kujifunza kuhusu mambo ya kimataifa kama sehemu ya urithi wa kazi yetu.“

Kutimiza haya malengo tunafanya yafuatayo;

  • Tumefanya kazi yetu ya elimu kuwa ya kimataifa.
  •  Kuunganisha kazi yetu na washirika wote kwenye shule nan je ya shule.
  •  Kufanya kazi na makundi ya malengo yanayohusisha makundi ya umri tofauti na mazingira tofauti.

Mwelekeo wa kimataifa:

Wote Tanzania na ujerumani tuna nia.Nchini Ujerumani tupo kwa ajili ya taasisi za elimu kama taasisi ya ushirika;Tunatoa ofa za elimu,vifaa vya elimu na kuandaa matukio kwa umma ambayo yanashughulika na biashara ya haki,matumizi endelevu na majukumu ya dunia kutokana na kanuni zinazotuongoza.Hizi ofa zinatakiwa ziwe kwa njia ambayo washiriki wanaweza kuelewa.Kwa mfano, kuweza kupata taswira ya taarifa kamili kwenye eneo halisi.Washiriki wanatakiwa kuwa na fursa ya kupata uzoefu kwenye mada husika ya tukio kama vile kuhusu kahawa.

Nchini Tanzania fikira kuhusu mambo endelevu ni lengo kuu la kazi yetu ya elimu.Tunajaribu kukuza uelewa wa mazingira kwa kizazi kichanga cha watanzania,kwa upande mmoja kuwa na uzoefu na mazingira na kwa upande mwingine kupitia mambo tunayoyatoa kwenye shule ya sekondari KIUMAKO.kwenye mada hii tunaandaa safari kwa wanafunzi ambazo zinawafanya kwa njia moja wawe na uzoefu na mazingira na kwa njia nyingine inatoa maelezo kuhusu maeneo fulani ya utunzaji wa mazingira na maisha endelevu na uchumi,kwa mfano kwa kuonyesha njia za kutunza mazingira na utunzaji endelevu na utumiaji wa makini wa mbao.
Zaidi ya hayo tunafanyakazi na mwongozo wa kupanda miti unaosema:Tunapanda miti kwa kila mwanafunzi anayefundishwa kwenye shule ya sekondari KIUMAKO.lwa kufanya hivi tunataka kukuza uelewa wa umuhimu wa matumizi endelevu ya rasilimali kwa ujumla.

Mtandao:

Ni lengo letu kujumuisha dhamira yetu kwa Tanzania kwenye kazi za elimu nchini ujerumani.kwa sababu ya hili tunafanya kazi pamoja na taasisi nyingine ambazo zinashughulika na maswala ya elimu na tunajitahidi kuimarisha na kukuza matandao wetu kwa kukubali kushirikiana na wengine. Shule na pia vyuo na vituo visivyo vya kishule ni washiriki ambao wako sawa na tunaweza kujiunga nao.

Na makundi yaliyolegwa ya umri tofauti na mazingira tofauti:

Kwanza kabisa tunajaribu kutoa upatikanaji wa taarifa  halisi kupitia mawasiliano ya moja kwa moja na Tanzania au vifaa vyote vinavyohitajika kwa taasisi za elimu.Hizi zinaweza kuwa picha,vitambaa,vinyago au vifaa vya kila siku na pia kahawa mbichi au katani kama zao la kilimo.Haya mabadilishano ya moja kwa moja yanatakiwa kubadilisha mtazamo kwenye maendeleo ya kimataifa kwa wanaojifunza. Kwenye mabadilishano haya tunafanya kazi na watu wa umri tofauti tofauti.

Tunatafuta ushirikiano na watoto wa chekechea na pia watoto wa shule,wanafunzi na watu wazima.

Tunaandaa matukio na kazi zote kwenye taasisi husika na pia kwa umma.

Tunazuia ufundishaji wa jadi kwenye madarasa na kuchagua kutumia njia ya kufanya kazi kwa uzoefu ambayo inaleta maana.

 

 

 

 

Nyuma