Mazingra

Eneo la Moshi liko kaskazini mwa Tanzania kwenye safu ya mlima Kilimanjaro karibu na mpaka wa Kenya. Kuna hali ya hewa ya joto ila kwa sababu ya mlima Kilimanjaro sio joto sana.shule yetu ipo katika urefu wa mita 1600 juu ya usawa wa bahari. Na mazingira yake ni ya kijani sana na ni mazingira mazuri sana. Wakazi wengi wanaishi katika nyumba za matofali na wana umeme na maji.

Eneo lililoko mita chache chini ya hapa liko wazi Zaidi na kuna mimea michache na joto zaidi. Kwenye mitaa ya karibu unakuta watu maskini ambao wengi wao bado wanaishi kwenye nyumba za udongo.