Malazi
Vijana wetu wa kujitolea wanaishi kwenye nyumba ya wageni ya familia ambayo mmiliki wake ana uhusiano wa karibu sana na KIUMAKO. Mama mwenye nyumba Pracseda anafanya kazi kwenye ofisi ya shule na mume wake Gilbert anaweza kufanya karibia kila kitu na ni mpangaji mzuri sana ambaye kila mtu anafaidika nae.
Kwa sasa kuna ofisi ya vijana wetu wa kujitolea na pia sehemu ambayo hawa vijana wanaweza kufanya kazi na kuhifadhi vitu vyao.
Kwenye hii nyumba nzuri ya wageni watu wote wanasaidiana kupika na kazi za nyumbani zinagawanywa.Chakula kinachopikwa ni cha kitanzania.