Kanuni zinazo tuongoza

Kutokana na mahitaji ya agenda ya 21. Binadamu wanatakiwa kuwezeshwa kuweza kupambana na changamoto za utandawazi na kutengeneza dunia kwa kutumia elimu kuhakikisha maendeleo endelevu.

RAFIKI e.v. inahisi kuwa ina wajibu kwenye agenda ya 21 na ni lengo letu kujumuisha mambo ya kujifunza kuhusu mambo ya kimataifa kama sehemu ya urithi wa kazi yetu.

Tunafanya kazi bega kwa bega na washirika wetu wa Tanzania kwa usawa. Miradi ya Tanzania inapendekezwa na kutekelezwa na washirika wetu.sisi tunahamasisha utoaji wa fedha na kugharamia miradi hiyo pamoja na kutoa ushauri kwa washirika wetu. Kazi yetu inatambulishwa na kanuni ya mambo endelevu na biashara ya haki.kwa ujumla na kabla ya yote nchini Tanzania tunasimamia usawa wa jinsia kwenye jamii kwa mfano kuwahamasisha wanawake kwenye kazi na pia na pia kushiriki kwa usawa kwenye  maisha ya jamii kama michezo.

Panapowezekana tunajaribu kuwasaidia watanzania kuanzisha maisha ya kujitegemea wenyewe kufedha.

Ili kukabiliana na kukosekana kwa usawa na kuwa na udhalimu kwenye dunia yetu mabadiliko makubwa kwenye tabia,kama inawezekana hata mabadiliko kwenye mifumo inayoendelea yanahitajika.kwa kufundisha tunataka kuchangia kwenye mabadiliko ya kujitambua kwa sababu hii ni chanzo cha kubadilika kwa tabia.

RAFIKI e.V. inafanya kazi kama shirika lisilopata faida na halijiingizi kwenye mambo ya kutaka kujipatia fedha .

Kwa mambo yafuatayo tunajaribu kufikia  malengo yetu:

  • Ujenzi na uendelezaji wa shule ya sekondari Mrimbo/Tanzania.
  • Maendeleo ya mada ya elimu iliyo na msingi wa mafanikio ya kiuchumi endelevu kwa shule hiyo.
  • Kwa kushirikiana na mashirika mengine na taasisi za elimu.
  • Kwa kuandaa ziara.
  •  Kwa kuandaa matukio ambayo yanatoa taarifa ambazo zinatangaza shirika letu ,kazi zetu,biashara ya haki na mbinu endelevu za uzalishaji.
  • Kwa kukuza mfuko wetu wa fedha ili kuweza kufadhili miradi yetu.
  • Kwa kutangaza Tanzania,shirika letu na miradi yetu kupitia mahusiano ya umma.

Dondoo:

“Uhuru na usawa- Hizi ni thamani ambazo tunatakiwa kuwa nazo kama tunataka kupeleka utandawazi kwenye njia nzuri kiuchumi na kisiasa”.

Johannes Rau

“Wote tunashiriki changamoto kubwa kwa wakati wetu :Kulinda amani,kuhifadhi uumbaji na kupambana na umasikini. Umasikini ukiwa popote unajenga hatari kwa wanadamu kila mahali”.

Richard von Weizsäcker

 

 

 

 

 

Nyuma